Hatimaye
mwimbaji wa nyimbo za injili Moses Yonah anayetamba na
Album inayotambulika kwa jina la
Ee BWANA
UINULIWE Amesema kuwa alikuwa kama yuko
shimoni kutokana na changamoto mbalimbali alizopitia ili kufikia kukamilisha
Album yake . Akiongea na jarida hili
Moses Yonah alisema kuwa kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji imekuwa ndoto yake ya muda mrefu sana tangu akiwa
mototo, pamoja na kuwa na ndoto hiyo kwa muda mrefu hakuwa na budi kusubiri na
kuvumilia nyakati ngumu alizokutana nazo na hapa namnukuu;
“ Kwanza kabisa
nimshukuru MUNGU wetu mwenye kuwarehemu maelfu elfu wamtafutao, kwangu ni kama
nimetoka shimoni kutokana kule nilikotoka na yale niliyopitia, nimesaidia
waimbaji wengi ambao wamekuwa leo hii ni
waimbaji maarufu waliponiomba kuwafundisha kuimba. Lakini hilo halikuweza
kurahisisha njia yangu ya kufikia ile ndoto yangu ya kumtumikia MUNGU kwa
kufanya kazi yangu mwenyewe. Nilitegemea kuwa huenda wale niliowasaidia
wangeweza kunishika mkono, lakini MUNGU kwa mapenzi yake haikuwa hivyo, na leo
hii nimefanikiwa kuifikia ndoto yangu, najiona kama nimetoka ndani ya shimo
refu sana”
Akiongelea kuhusu ujio wa album yake yenye nyimbo zenye
mguso wa kimungu, Moses alisema kuwa kwa
yote yaliyomo katika album yake ni kwa neema tu ya MUNGU, na wala si kwa uwezo wake yeye hii hapa nukuu
nyingine ya kile alichosema.
“Mimi ukiniuliza
kuwa ulifikiria nini hadi kuandika wimbo wa namna hii, kwa kweli jibu lake ni
gumu sana na siwezi kujua nini nikujibu, maana nilikuwa najikuta tu naanza
kuimba na kisha naunakili wimbo huo
kwenye karatasi, naweza kusema
kuwa ni MUNGU mwenyewe maana kwa uwezo wangu nisingeweza kufanya hayo. Ninachoweza kukumbuka ni kwamba, nimekuwa
nikimwomba sana Mungu aniongoze katika kile ninachonia kukifanya”
Moses Yonah anatarajia kufanya uzinduzi wa album yake hivi
karibuni mara tu baada ya maandalizi yote ya kazi husika kuwa yamekamilika na amewataka wapenzi wote wa wa nyimbo za Injili Tanzania na nje ya
Tanzania wa DINI zote, wajiandae kupokea kazi ambayo itawajenga na kuwaimarisha
kiroho.
Mawasiiano
MOSES YONAH
+255 656 657639
Dar es salaam - TZ