Friday, December 15, 2017

SHEDRACK SHERIA KUINGIA SOKONI KWA KISHINDO

    Mwimbaji mahiri wa nyimbo za njili Tanzania Shedrack Sheria maarufu kwa jina la TUTALIPWA amesema kuwa anajipanga kuingia sokoni kwa kishindo kikubwa baada ya kukamilisha mipango yote ya kuingiza kazi yake sokoni. Akiongea na jarida hili mwimbaji huyo alisema kuwa amejipanga vilivyo kukabiliana na panda shuka zote za sokoni. Alipoulizwa kuhusu kampuni ambayo itamsambazia kazi yake alisema kuwa hajafikiria kusambaziwa kazi yake na kampuni yoyote ile maana anao uwezo wa kufanya hivyo yeye mwenyewe. Na hapa namnukuu

"Waimbaji wengi hawajui thamani ya huduma zao, wanakimbilia kuuza haki milki zao kwa wasambazaji jambo ambalo lina wafanya wengi wako kuona kama huduma hii ni biashara ya kuuza na kununua, hii ni kazi ya MUNGU hivyo sipaswi kuhangaisha sana akili yangu kuwa niisambaze vipi. Mungu mwenye ataisimamia kazi yake ili iweze kufika mahali inapostahili, Mungu ameniita ili nimtumikie, hivyo sinabudi kujipanga mimi mwenyewe kujua ni jinsi gani nitaipeleka injili"

       Na alipoulizwa na jarida hili kuhusu namna atakavyo ilinda kazi yake juu ya uharamia wa kazi za wasanii alisema kuwa yeye kwa kuliona hilo kama ni tatizo ambalo linasumbua wengi. Alisema amejipanga kikamilifu na haya ndiyo maneno yake "Mimi nilijua kuwa hilo ni changamoto ambayo iko mbele yangu, lakini  mimi kwa kulifahamu hilo, kazi zangu zote nimezisajiri na zinalindwa kisheria chini chama cha haki milki Tanzania (COSOTA)" Album yake ya TUTALIPWA inajumla ya nyimbo nane (8) ambazo zote zimefanya vizuri sana katika vituo mbalimbali vya TV hapa nchini.

No comments:

Post a Comment