Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili Tanzania Shedrack Sheria ameweka wazi mikakati yake katika huduma ya uimbaji. Akiongea hayo na Joyland Pictures msanii huyo ambaye anazidi kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na album yake ya TUTALIPWA ambayo aliizindua mwezi wa October mwaka huu. Amesema kuwa yeye yuko kinyume kabisa na mitazamo wa waimbaji wengi wa nyimbo za injili ambao wamejikita zaidi katika kutafuta fedha hapa namnukuu "Mimi sifanyi huduma kwa ajili ya mkate, mimi namtumikia Mungu kama alivyotuagiza, na chochote ninachokipata kupitia huduma yangu ya uimbaji sikihesabu kama ujira. Bali kama matunda tu ya huduma ambayo Bwana amenipa" Aliongeza kusema kuwa kama ni habari ya kusaka mafanikio yeye anao uwezo wa kufanya kazi mbalimbali nje na huduma. Hivyo kazi anazozifanya zinatosha kumpa kipato ambacho kitamsaidia kuendesha maisha yake. Pia aliongeza kusema kuwa hawezi kuweka dau la pesa ili kuhudumu mahali, bali akiwa na nafasi kulingana nanratiba yake ya kazi zake za kujipatia kipato. Atakwenda kuhudumu pasipo kutegemea ujira kutoka kwa aliomwita kuhudumu aliongeza kusema. Namnukuu "Ujue tunakosea sana tunapogeuza huduma ya Bwana kama njia ya kutuweka mjini, hakuna maandiko ambayo yanatuagiza kuweke madau ya fedha ndipo tukaifanye kazi ya Bwana". Kuhusu suala la kusaidia wasanii wachanga, alisema anajipanga kuanza kuwasaidia kwa kadili ya uwezo atakao kuwa nao kupitia LEBO yake mpya ya TUTALIPWA PROMOTION.
No comments:
Post a Comment