Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili Tanzania Shedrack Sheria hatimaye ameweza kuitekeleza ile ahadi yake ya kuwasaidia wasanii chipukizi aliyoitoa kwenye
uzinduzi wa album yake TUTALIPWA inayofanya vema kwa sasa. Siku ya uzinduzi wa
album hiyo msanii huyo alitoa ahadi yake mbele ya mamia ya watu waliokuwa wamejaa
ukumbini siku hiyo kuwa uzinduzi wa album hiyo ulikuwa ni kwa lengo la
kuwasaidia wasanii chipukizi kufika
malengo makubwa ya hudumu ikiwa ni pamoja na kuweza kuwafadhiri kufanya video bora na zenye ushawishi kwa jamii. Kwa
kulitambua hilo Shedrack Sheria
amefungua ukurasa mpya kwa kuanzisha kampeni yake ya kuwasaidia wasanii
chipukizi kupitia LEBO ya TUTALIPWA PROMOTION. Akizungumzia kuwasaidia wasanii chipukizi alikuwa na haya
ya kusema na hapa namnukuu
“TUTALIPWA PROMOTION ni Lebo mahususi kwa ajili ya kusaidia wasanii
chipukizi ambao wameshindwa kufikia malengo yao. Mimi binafsi nimepitia huko
nimehangaika sana kutafuta msaada na nimekutana na changamoto nyingi sana za
kukatisha tamaa na kuvunja moyo pia. Kwa kulitambua hilo nimeamua kuwashika
mkono kaka zangu na dada zangu ili kuvuka ukuta mrefu ulio mbele yao, ni kweli
nafamahu kuwa Tanzania tunao waimbaji wazuri sana, pengine hata kuzidi hawa
ambao tayari wameshaonekana, lakini tatizo linatokea tu ambapo wanakuwa
hawawezi kufikia malengo yao kutokana na changamoto mbalimbali za kimaisha
wanazopitia maishani, kwa neema ya Bwana, lebo ya TUTALIPWA PROMOTION
itawasaidia kadiri ya uwezo wake kufikia malengo yao,,
Lebo hii ya TUTALIPWA PROMOTION inajikita zaidii katika kuwasaidia waimbaji
chipukizi wa nyimbo za injli kuweza kufanya
Video bora zenye kukidhi viwango vya soko la ndani na nje ya nchi. Ili
kuweza kunufaika na fursa hii msanii chipukizi wa nyimbo za injili anapaswa
kuwa tayari awe amekwisha rekodi nyimbo
zake na ziwe tayari. Lebo ya TUTALIPWA
inatoa ufadhiri upande wa video na siyo upande wa kurekodi nyimbo, hii
inatokana kwamba gharama za kuingia studio na kurekodi nyimbo zimekuwa za
kawaida ambazo kila mmoja amekuwa akizimudu. Ukilinganisha na changamoto kubwa
katika kuandaa vieo, ambapo gharama zake
huwa ni kubwa mara dufu. Hii ni moja
kati ya fursa nadra sana kuwahi kutokea katika huduma hii ya uimbaji. Lengo kuu
ni kuwainua wasanii chipukizi na si vinginevyo, lebo hii inasimamia maagizo ya
Mungu ya kusidiana na kuinuana katika upendo wa kristo. Huduma hii haibagui
mwimbaji kutoka na dhehebu lake, bali
kwa pamoja wote waliojitoa kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji , wanayo nafasi
ya kusaidiwa kuyafikia malengo yao. Lebo ya TUTALIPWA PROMOTION ipo kwa ajili ya kusaidia kwa njia ya upendo
kuifikia ile ndoto yao ya siku nyingi ambayo imekuwa ikiwajilia na hii hii
ndiyo fursa yako.
Jambo la kufanya
mara upatapo ujumbe huu ni kupiga simu kwa kutumia namba ambazo zimetolewa hapo chini na kuongea moja kwa moja na
wasimamizi wa TUTALIPWA PROMOTION na hivyo utakuwa umepata nafasi ya jina lako
kuingizwa kwenye orodha ya waimbaji ambao watakuwa wakifanyiwa tathimini kazi
zao kwa ajili ya kufanyiwa VIDEO
kuanzia mwanzoni mwa mwezi JANUARY
2018. Pia TUTALIPWA PROMOTION itakusaidia kujifunza mambo mbalimbali ya
huduma ya uimbaji ili kukuwezesha kufanya huduma yako katika viwango vinavyostahili.
Usichelewe maana wahitaji ni wengi.
Mungu wa Mbinguni na akubariki na akufanikishe zaidi.
Mawasailianao
TUTALIPWA PROMOTION
CONT: +255 652 776 936
+255 789 972 333
Dar es salaam - Tanzania
No comments:
Post a Comment