Tuesday, January 2, 2018

NIMETOKA SHIMONI

       Hatimaye mwimbaji  wa  nyimbo za injili Moses Yonah anayetamba na Album inayotambulika kwa jina la
 Ee BWANA UINULIWE  Amesema kuwa alikuwa kama yuko shimoni kutokana na changamoto mbalimbali alizopitia ili kufikia kukamilisha Album yake . Akiongea na jarida  hili Moses Yonah alisema kuwa kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji  imekuwa ndoto yake ya muda mrefu sana tangu akiwa mototo, pamoja na kuwa na ndoto hiyo kwa muda mrefu hakuwa na budi kusubiri na kuvumilia nyakati ngumu alizokutana nazo na hapa namnukuu;

“ Kwanza kabisa nimshukuru MUNGU wetu mwenye kuwarehemu maelfu elfu wamtafutao, kwangu ni kama nimetoka shimoni kutokana kule nilikotoka na yale niliyopitia, nimesaidia waimbaji wengi ambao  wamekuwa leo hii ni waimbaji maarufu waliponiomba kuwafundisha kuimba. Lakini hilo halikuweza kurahisisha njia yangu ya kufikia ile ndoto yangu ya kumtumikia MUNGU kwa kufanya kazi yangu mwenyewe. Nilitegemea kuwa huenda wale niliowasaidia wangeweza kunishika mkono, lakini MUNGU kwa mapenzi yake haikuwa hivyo, na leo hii nimefanikiwa kuifikia ndoto yangu, najiona kama nimetoka ndani ya shimo refu sana”

Akiongelea kuhusu ujio wa album yake yenye nyimbo zenye mguso wa kimungu, Moses alisema kuwa  kwa yote yaliyomo katika album yake ni kwa neema tu ya MUNGU,  na wala si kwa uwezo wake yeye hii hapa nukuu nyingine ya kile alichosema.

“Mimi ukiniuliza kuwa ulifikiria nini hadi kuandika wimbo wa namna hii, kwa kweli jibu lake ni gumu sana na siwezi kujua nini nikujibu, maana nilikuwa najikuta tu naanza kuimba na kisha naunakili wimbo huo  kwenye karatasi, naweza  kusema kuwa ni MUNGU mwenyewe maana kwa uwezo wangu nisingeweza kufanya hayo.  Ninachoweza kukumbuka ni kwamba, nimekuwa nikimwomba sana Mungu aniongoze katika kile ninachonia kukifanya”

Moses  Yonah  anatarajia kufanya uzinduzi wa album yake hivi karibuni mara tu baada ya maandalizi yote ya kazi  husika kuwa yamekamilika na amewataka wapenzi  wote wa  wa nyimbo za Injili Tanzania na nje ya Tanzania wa DINI zote, wajiandae kupokea kazi ambayo itawajenga na kuwaimarisha kiroho.

Mawasiiano
MOSES YONAH
+255 656 657639
Dar es salaam - TZ