Sunday, December 17, 2017

NEEMA KWA WAIMBAJI CHIPUKIZI WA MUSIC WA INJILI TZ.

         Mwimbaji  mahiri wa nyimbo  za injili Tanzania Shedrack Sheria  hatimaye ameweza kuitekeleza ile ahadi yake ya  kuwasaidia wasanii chipukizi aliyoitoa kwenye uzinduzi wa album  yake TUTALIPWA  inayofanya vema kwa sasa. Siku ya uzinduzi wa album hiyo msanii huyo alitoa ahadi yake mbele ya mamia ya watu waliokuwa wamejaa ukumbini siku hiyo kuwa uzinduzi wa album hiyo ulikuwa ni kwa lengo la kuwasaidia  wasanii chipukizi kufika malengo makubwa ya hudumu ikiwa ni pamoja na kuweza kuwafadhiri kufanya  video bora na zenye ushawishi kwa jamii. Kwa kulitambua hilo Shedrack Sheria amefungua ukurasa mpya kwa kuanzisha kampeni yake ya kuwasaidia wasanii chipukizi kupitia LEBO ya TUTALIPWA PROMOTION. Akizungumzia  kuwasaidia wasanii chipukizi alikuwa na haya ya kusema na hapa namnukuu

“TUTALIPWA PROMOTION ni Lebo mahususi kwa ajili ya kusaidia wasanii chipukizi ambao wameshindwa kufikia malengo yao. Mimi binafsi nimepitia huko nimehangaika sana kutafuta msaada na nimekutana na changamoto nyingi sana za kukatisha tamaa na kuvunja moyo pia. Kwa kulitambua hilo nimeamua kuwashika mkono kaka zangu na dada zangu ili kuvuka ukuta mrefu ulio mbele yao, ni kweli nafamahu kuwa Tanzania tunao waimbaji wazuri sana, pengine hata kuzidi hawa ambao tayari wameshaonekana, lakini tatizo linatokea tu ambapo wanakuwa hawawezi kufikia malengo yao kutokana na changamoto mbalimbali za kimaisha wanazopitia maishani, kwa neema ya Bwana, lebo ya TUTALIPWA PROMOTION itawasaidia kadiri ya uwezo wake kufikia malengo yao,,

      Lebo hii ya TUTALIPWA PROMOTION inajikita zaidii katika kuwasaidia waimbaji chipukizi wa nyimbo za injli kuweza kufanya  Video bora zenye kukidhi viwango vya soko la ndani na nje ya nchi. Ili kuweza kunufaika na fursa hii msanii chipukizi wa nyimbo za injili anapaswa kuwa tayari awe amekwisha rekodi  nyimbo zake na ziwe tayari. Lebo ya TUTALIPWA inatoa ufadhiri upande wa video na siyo upande wa kurekodi nyimbo, hii inatokana kwamba gharama za kuingia studio na kurekodi nyimbo zimekuwa za kawaida ambazo kila mmoja amekuwa akizimudu. Ukilinganisha na changamoto kubwa katika kuandaa vieo,  ambapo gharama zake huwa ni kubwa mara dufu.  Hii ni moja kati ya fursa nadra sana kuwahi kutokea katika huduma hii ya uimbaji. Lengo kuu ni kuwainua wasanii chipukizi na si vinginevyo, lebo hii inasimamia maagizo ya Mungu ya kusidiana na kuinuana katika upendo wa kristo. Huduma hii haibagui mwimbaji kutoka na dhehebu lake,  bali kwa pamoja wote waliojitoa kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji , wanayo nafasi ya kusaidiwa kuyafikia malengo yao. Lebo ya TUTALIPWA  PROMOTION  ipo kwa ajili ya kusaidia kwa njia ya upendo kuifikia ile ndoto yao ya siku nyingi ambayo imekuwa ikiwajilia na hii hii ndiyo fursa yako.
   Jambo la kufanya mara upatapo ujumbe huu ni kupiga simu kwa kutumia namba ambazo zimetolewa  hapo chini na kuongea moja kwa moja na wasimamizi wa TUTALIPWA PROMOTION na hivyo utakuwa umepata nafasi ya jina lako kuingizwa kwenye orodha ya waimbaji ambao watakuwa wakifanyiwa tathimini kazi zao kwa ajili ya  kufanyiwa VIDEO  kuanzia mwanzoni  mwa mwezi  JANUARY  2018. Pia TUTALIPWA PROMOTION itakusaidia kujifunza mambo mbalimbali ya huduma ya uimbaji ili kukuwezesha kufanya huduma yako katika viwango vinavyostahili. Usichelewe maana wahitaji ni wengi.  Mungu wa Mbinguni na akubariki na akufanikishe zaidi.






Mawasailianao
TUTALIPWA PROMOTION
CONT: +255 652  776 936
+255 789 972 333
Dar es salaam - Tanzania




Friday, December 15, 2017

SHEDRACK SHERIA KUINGIA SOKONI KWA KISHINDO

    Mwimbaji mahiri wa nyimbo za njili Tanzania Shedrack Sheria maarufu kwa jina la TUTALIPWA amesema kuwa anajipanga kuingia sokoni kwa kishindo kikubwa baada ya kukamilisha mipango yote ya kuingiza kazi yake sokoni. Akiongea na jarida hili mwimbaji huyo alisema kuwa amejipanga vilivyo kukabiliana na panda shuka zote za sokoni. Alipoulizwa kuhusu kampuni ambayo itamsambazia kazi yake alisema kuwa hajafikiria kusambaziwa kazi yake na kampuni yoyote ile maana anao uwezo wa kufanya hivyo yeye mwenyewe. Na hapa namnukuu

"Waimbaji wengi hawajui thamani ya huduma zao, wanakimbilia kuuza haki milki zao kwa wasambazaji jambo ambalo lina wafanya wengi wako kuona kama huduma hii ni biashara ya kuuza na kununua, hii ni kazi ya MUNGU hivyo sipaswi kuhangaisha sana akili yangu kuwa niisambaze vipi. Mungu mwenye ataisimamia kazi yake ili iweze kufika mahali inapostahili, Mungu ameniita ili nimtumikie, hivyo sinabudi kujipanga mimi mwenyewe kujua ni jinsi gani nitaipeleka injili"

       Na alipoulizwa na jarida hili kuhusu namna atakavyo ilinda kazi yake juu ya uharamia wa kazi za wasanii alisema kuwa yeye kwa kuliona hilo kama ni tatizo ambalo linasumbua wengi. Alisema amejipanga kikamilifu na haya ndiyo maneno yake "Mimi nilijua kuwa hilo ni changamoto ambayo iko mbele yangu, lakini  mimi kwa kulifahamu hilo, kazi zangu zote nimezisajiri na zinalindwa kisheria chini chama cha haki milki Tanzania (COSOTA)" Album yake ya TUTALIPWA inajumla ya nyimbo nane (8) ambazo zote zimefanya vizuri sana katika vituo mbalimbali vya TV hapa nchini.

Wednesday, December 13, 2017

SITEGEMEI PESA YA MIALIKO KUISHI.

      Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili Tanzania Shedrack Sheria ameweka wazi  mikakati yake katika huduma ya uimbaji. Akiongea hayo na Joyland Pictures msanii huyo ambaye anazidi kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na album yake ya TUTALIPWA ambayo aliizindua mwezi wa October mwaka huu. Amesema kuwa yeye yuko kinyume kabisa na mitazamo wa waimbaji wengi wa nyimbo za injili ambao wamejikita zaidi katika kutafuta fedha hapa namnukuu "Mimi sifanyi huduma kwa ajili ya mkate, mimi namtumikia Mungu kama alivyotuagiza, na chochote ninachokipata kupitia huduma yangu ya uimbaji sikihesabu kama ujira. Bali kama matunda tu ya huduma ambayo Bwana amenipa" Aliongeza kusema kuwa kama ni habari ya kusaka  mafanikio yeye anao uwezo wa kufanya kazi mbalimbali nje na huduma. Hivyo kazi anazozifanya zinatosha kumpa kipato ambacho kitamsaidia kuendesha maisha yake. Pia aliongeza kusema kuwa hawezi kuweka dau la pesa ili kuhudumu mahali, bali akiwa na nafasi kulingana nanratiba yake ya kazi zake za kujipatia kipato. Atakwenda kuhudumu pasipo kutegemea ujira kutoka kwa aliomwita kuhudumu aliongeza kusema. Namnukuu "Ujue tunakosea sana tunapogeuza huduma ya Bwana kama njia ya kutuweka mjini, hakuna maandiko ambayo yanatuagiza kuweke madau ya fedha ndipo tukaifanye kazi ya Bwana". Kuhusu suala la kusaidia wasanii wachanga, alisema anajipanga kuanza kuwasaidia kwa kadili ya uwezo atakao kuwa nao kupitia LEBO yake mpya ya TUTALIPWA PROMOTION.




UJIO MPYA WA ALBUM MPYA YA SARAH ABEL

      Mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania Sarah Abel ameachia album mpya ya nyimbo za Injili inayoenda kwa jina la NI BWANA. Akiongea na Joyland Pictures ameielezea album hiyo kuwa ni album ya kipekee ambayo imebeba nyimbo (9) zenye mafundisho. Zinazojenga na kuelimisha jamii. Amewataka watanzania  wote kujipatia nakala ya album hiyo ambayo haitawaacha kama walivyo. Bali itawajenga na kuwafanya upya kiroho na kimwili.