Thursday, June 4, 2020
MWANA WA DAUDI AELEZEA CHANGAMOTO ALIZOPITIA
Mwimbaji wa nyimbo za Injili TZ #SAMSON #MWANA WA #DAUDI anayefanya vema na album yake inayoitwa #NAMI #NITANG'ARA ameelezea changamoto mbalimbali alizopitia hadi kufikia hatua ya kufanya video ya album yake. Samson amesema kuwa amepitia magumu mengi ikiwemo kukosa mtu wa kumwelekeza njia ya kufikia malengo yake na hii hapa ni nukuu yake "Kusema kwelli nimehangaika sana kutafuta mtu wa kunishika mkono. Nimezunguka sana na kujaribu kila njia nikitafuta kufikia maono ya kuwa na video yangu. Wengi walinipa kisogo lakini sikukata tamaa. Niliamua kumtegemea Mungu kwa kuomba usiku na mchana. Mungu alisikia kilio changu na kunikutanisha na Dir. Lenny na kupitia yeye nimeweza kufikia maono yangu" Mwisho wa kunukuu. Amewataka waimbaji wenzake kutokukata tamaa wanapokutana na changamoto za kihuduma.
Kwa maelezo zaidi kuhusu ujio wa Album hii mpya, endelea kufuatilia matangazo kupitia blog hii.
STEPHANO MWANA WA MWINYI KUACHIA ALBUM MPYA
Mwimbaji wa nyimbo za Injili TZ #STEPHANO #MWANA WA #MWINYI nataraji akuachia Album yake ya nyimbo za injili inayoitwa #MUNGU WA #MATENGENEZO, albbum
Album yake tayari imeshakamilika na kitu anachosubiri hivi sasa ni Janga la #COVID-19 kupita. Album hii imesheheni nyimbo zenye mguso wa roho Mtakatifu zitakazokusogeza kwenye uwepo.
Usipange kuikosa nakala yako!! Anawaomba watu wote kuwa tayari kuipokea album hii ambayo itafanyika baraka kubwa katika maisha.
Kwa maelezo zaidi kuhusu ujio wa Album hii mpya, endelea kufuatilia matangazo kupitia blog hii.
Tuesday, January 2, 2018
NIMETOKA SHIMONI
Hatimaye
mwimbaji wa nyimbo za injili Moses Yonah anayetamba na
Album inayotambulika kwa jina la
Ee BWANA
UINULIWE Amesema kuwa alikuwa kama yuko
shimoni kutokana na changamoto mbalimbali alizopitia ili kufikia kukamilisha
Album yake . Akiongea na jarida hili
Moses Yonah alisema kuwa kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji imekuwa ndoto yake ya muda mrefu sana tangu akiwa
mototo, pamoja na kuwa na ndoto hiyo kwa muda mrefu hakuwa na budi kusubiri na
kuvumilia nyakati ngumu alizokutana nazo na hapa namnukuu;
“ Kwanza kabisa
nimshukuru MUNGU wetu mwenye kuwarehemu maelfu elfu wamtafutao, kwangu ni kama
nimetoka shimoni kutokana kule nilikotoka na yale niliyopitia, nimesaidia
waimbaji wengi ambao wamekuwa leo hii ni
waimbaji maarufu waliponiomba kuwafundisha kuimba. Lakini hilo halikuweza
kurahisisha njia yangu ya kufikia ile ndoto yangu ya kumtumikia MUNGU kwa
kufanya kazi yangu mwenyewe. Nilitegemea kuwa huenda wale niliowasaidia
wangeweza kunishika mkono, lakini MUNGU kwa mapenzi yake haikuwa hivyo, na leo
hii nimefanikiwa kuifikia ndoto yangu, najiona kama nimetoka ndani ya shimo
refu sana”
Akiongelea kuhusu ujio wa album yake yenye nyimbo zenye
mguso wa kimungu, Moses alisema kuwa kwa
yote yaliyomo katika album yake ni kwa neema tu ya MUNGU, na wala si kwa uwezo wake yeye hii hapa nukuu
nyingine ya kile alichosema.
“Mimi ukiniuliza
kuwa ulifikiria nini hadi kuandika wimbo wa namna hii, kwa kweli jibu lake ni
gumu sana na siwezi kujua nini nikujibu, maana nilikuwa najikuta tu naanza
kuimba na kisha naunakili wimbo huo
kwenye karatasi, naweza kusema
kuwa ni MUNGU mwenyewe maana kwa uwezo wangu nisingeweza kufanya hayo. Ninachoweza kukumbuka ni kwamba, nimekuwa
nikimwomba sana Mungu aniongoze katika kile ninachonia kukifanya”
Moses Yonah anatarajia kufanya uzinduzi wa album yake hivi
karibuni mara tu baada ya maandalizi yote ya kazi husika kuwa yamekamilika na amewataka wapenzi wote wa wa nyimbo za Injili Tanzania na nje ya
Tanzania wa DINI zote, wajiandae kupokea kazi ambayo itawajenga na kuwaimarisha
kiroho.
Mawasiiano
MOSES YONAH
+255 656 657639
Dar es salaam - TZ
Sunday, December 17, 2017
NEEMA KWA WAIMBAJI CHIPUKIZI WA MUSIC WA INJILI TZ.
Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili Tanzania Shedrack Sheria hatimaye ameweza kuitekeleza ile ahadi yake ya kuwasaidia wasanii chipukizi aliyoitoa kwenye
uzinduzi wa album yake TUTALIPWA inayofanya vema kwa sasa. Siku ya uzinduzi wa
album hiyo msanii huyo alitoa ahadi yake mbele ya mamia ya watu waliokuwa wamejaa
ukumbini siku hiyo kuwa uzinduzi wa album hiyo ulikuwa ni kwa lengo la
kuwasaidia wasanii chipukizi kufika
malengo makubwa ya hudumu ikiwa ni pamoja na kuweza kuwafadhiri kufanya video bora na zenye ushawishi kwa jamii. Kwa
kulitambua hilo Shedrack Sheria
amefungua ukurasa mpya kwa kuanzisha kampeni yake ya kuwasaidia wasanii
chipukizi kupitia LEBO ya TUTALIPWA PROMOTION. Akizungumzia kuwasaidia wasanii chipukizi alikuwa na haya
ya kusema na hapa namnukuu
“TUTALIPWA PROMOTION ni Lebo mahususi kwa ajili ya kusaidia wasanii
chipukizi ambao wameshindwa kufikia malengo yao. Mimi binafsi nimepitia huko
nimehangaika sana kutafuta msaada na nimekutana na changamoto nyingi sana za
kukatisha tamaa na kuvunja moyo pia. Kwa kulitambua hilo nimeamua kuwashika
mkono kaka zangu na dada zangu ili kuvuka ukuta mrefu ulio mbele yao, ni kweli
nafamahu kuwa Tanzania tunao waimbaji wazuri sana, pengine hata kuzidi hawa
ambao tayari wameshaonekana, lakini tatizo linatokea tu ambapo wanakuwa
hawawezi kufikia malengo yao kutokana na changamoto mbalimbali za kimaisha
wanazopitia maishani, kwa neema ya Bwana, lebo ya TUTALIPWA PROMOTION
itawasaidia kadiri ya uwezo wake kufikia malengo yao,,
Lebo hii ya TUTALIPWA PROMOTION inajikita zaidii katika kuwasaidia waimbaji
chipukizi wa nyimbo za injli kuweza kufanya
Video bora zenye kukidhi viwango vya soko la ndani na nje ya nchi. Ili
kuweza kunufaika na fursa hii msanii chipukizi wa nyimbo za injili anapaswa
kuwa tayari awe amekwisha rekodi nyimbo
zake na ziwe tayari. Lebo ya TUTALIPWA
inatoa ufadhiri upande wa video na siyo upande wa kurekodi nyimbo, hii
inatokana kwamba gharama za kuingia studio na kurekodi nyimbo zimekuwa za
kawaida ambazo kila mmoja amekuwa akizimudu. Ukilinganisha na changamoto kubwa
katika kuandaa vieo, ambapo gharama zake
huwa ni kubwa mara dufu. Hii ni moja
kati ya fursa nadra sana kuwahi kutokea katika huduma hii ya uimbaji. Lengo kuu
ni kuwainua wasanii chipukizi na si vinginevyo, lebo hii inasimamia maagizo ya
Mungu ya kusidiana na kuinuana katika upendo wa kristo. Huduma hii haibagui
mwimbaji kutoka na dhehebu lake, bali
kwa pamoja wote waliojitoa kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji , wanayo nafasi
ya kusaidiwa kuyafikia malengo yao. Lebo ya TUTALIPWA PROMOTION ipo kwa ajili ya kusaidia kwa njia ya upendo
kuifikia ile ndoto yao ya siku nyingi ambayo imekuwa ikiwajilia na hii hii
ndiyo fursa yako.
Jambo la kufanya
mara upatapo ujumbe huu ni kupiga simu kwa kutumia namba ambazo zimetolewa hapo chini na kuongea moja kwa moja na
wasimamizi wa TUTALIPWA PROMOTION na hivyo utakuwa umepata nafasi ya jina lako
kuingizwa kwenye orodha ya waimbaji ambao watakuwa wakifanyiwa tathimini kazi
zao kwa ajili ya kufanyiwa VIDEO
kuanzia mwanzoni mwa mwezi JANUARY
2018. Pia TUTALIPWA PROMOTION itakusaidia kujifunza mambo mbalimbali ya
huduma ya uimbaji ili kukuwezesha kufanya huduma yako katika viwango vinavyostahili.
Usichelewe maana wahitaji ni wengi.
Mungu wa Mbinguni na akubariki na akufanikishe zaidi.
Mawasailianao
TUTALIPWA PROMOTION
CONT: +255 652 776 936
+255 789 972 333
Dar es salaam - Tanzania
Friday, December 15, 2017
SHEDRACK SHERIA KUINGIA SOKONI KWA KISHINDO
Mwimbaji mahiri wa nyimbo za njili Tanzania Shedrack Sheria maarufu kwa jina la TUTALIPWA amesema kuwa anajipanga kuingia sokoni kwa kishindo kikubwa baada ya kukamilisha mipango yote ya kuingiza kazi yake sokoni. Akiongea na jarida hili mwimbaji huyo alisema kuwa amejipanga vilivyo kukabiliana na panda shuka zote za sokoni. Alipoulizwa kuhusu kampuni ambayo itamsambazia kazi yake alisema kuwa hajafikiria kusambaziwa kazi yake na kampuni yoyote ile maana anao uwezo wa kufanya hivyo yeye mwenyewe. Na hapa namnukuu
"Waimbaji wengi hawajui thamani ya huduma zao, wanakimbilia kuuza haki milki zao kwa wasambazaji jambo ambalo lina wafanya wengi wako kuona kama huduma hii ni biashara ya kuuza na kununua, hii ni kazi ya MUNGU hivyo sipaswi kuhangaisha sana akili yangu kuwa niisambaze vipi. Mungu mwenye ataisimamia kazi yake ili iweze kufika mahali inapostahili, Mungu ameniita ili nimtumikie, hivyo sinabudi kujipanga mimi mwenyewe kujua ni jinsi gani nitaipeleka injili"
Na alipoulizwa na jarida hili kuhusu namna atakavyo ilinda kazi yake juu ya uharamia wa kazi za wasanii alisema kuwa yeye kwa kuliona hilo kama ni tatizo ambalo linasumbua wengi. Alisema amejipanga kikamilifu na haya ndiyo maneno yake "Mimi nilijua kuwa hilo ni changamoto ambayo iko mbele yangu, lakini mimi kwa kulifahamu hilo, kazi zangu zote nimezisajiri na zinalindwa kisheria chini chama cha haki milki Tanzania (COSOTA)" Album yake ya TUTALIPWA inajumla ya nyimbo nane (8) ambazo zote zimefanya vizuri sana katika vituo mbalimbali vya TV hapa nchini.
Wednesday, December 13, 2017
SITEGEMEI PESA YA MIALIKO KUISHI.
Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili Tanzania Shedrack Sheria ameweka wazi mikakati yake katika huduma ya uimbaji. Akiongea hayo na Joyland Pictures msanii huyo ambaye anazidi kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na album yake ya TUTALIPWA ambayo aliizindua mwezi wa October mwaka huu. Amesema kuwa yeye yuko kinyume kabisa na mitazamo wa waimbaji wengi wa nyimbo za injili ambao wamejikita zaidi katika kutafuta fedha hapa namnukuu "Mimi sifanyi huduma kwa ajili ya mkate, mimi namtumikia Mungu kama alivyotuagiza, na chochote ninachokipata kupitia huduma yangu ya uimbaji sikihesabu kama ujira. Bali kama matunda tu ya huduma ambayo Bwana amenipa" Aliongeza kusema kuwa kama ni habari ya kusaka mafanikio yeye anao uwezo wa kufanya kazi mbalimbali nje na huduma. Hivyo kazi anazozifanya zinatosha kumpa kipato ambacho kitamsaidia kuendesha maisha yake. Pia aliongeza kusema kuwa hawezi kuweka dau la pesa ili kuhudumu mahali, bali akiwa na nafasi kulingana nanratiba yake ya kazi zake za kujipatia kipato. Atakwenda kuhudumu pasipo kutegemea ujira kutoka kwa aliomwita kuhudumu aliongeza kusema. Namnukuu "Ujue tunakosea sana tunapogeuza huduma ya Bwana kama njia ya kutuweka mjini, hakuna maandiko ambayo yanatuagiza kuweke madau ya fedha ndipo tukaifanye kazi ya Bwana". Kuhusu suala la kusaidia wasanii wachanga, alisema anajipanga kuanza kuwasaidia kwa kadili ya uwezo atakao kuwa nao kupitia LEBO yake mpya ya TUTALIPWA PROMOTION.
UJIO MPYA WA ALBUM MPYA YA SARAH ABEL
Mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania Sarah Abel ameachia album mpya ya nyimbo za Injili inayoenda kwa jina la NI BWANA. Akiongea na Joyland Pictures ameielezea album hiyo kuwa ni album ya kipekee ambayo imebeba nyimbo (9) zenye mafundisho. Zinazojenga na kuelimisha jamii. Amewataka watanzania wote kujipatia nakala ya album hiyo ambayo haitawaacha kama walivyo. Bali itawajenga na kuwafanya upya kiroho na kimwili.
Subscribe to:
Posts (Atom)